Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA DAR ES SALAAM AGOSTI 27 HADI SEPTEMBA 4

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwataarifu wananchi kuwa Bunge la Afrika Mashariki litafanyika kuanzia Agosti 27 hadi Septemba 5 katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge hilo siku ya ufunguzi Agosti 27.

Vikao vya Bunge hilo vitakua vikifanyika kuanzia saa 8.30 mchana siku za Jumanne, Jumatano na Alhamis.

Katika kipindi cha wiki mbili EALA itapitia na kujadili ripoti mbalimbali na miswada mitatu. Miongoni mwa ripoti zitakazojadiliwa ni pamoja na ripoti ya kamati ya masuala ya jumuiya na upatanishi wa migogoro na Kituo cha uongozi cha Afrika cha Taasisi za Afrika Mashariki na Usalama wa jumuiya. Pia bunge litapokea taarifa  itakayojadiliwa  kutoka kamati ya masuala  ya Jumuiya na upatanishi wa migogoro juu ya hatua waliyofikia mpaka sasa.

Pia Ripoti nyingine ni kutoka kamati za kilimo, Utalii na Maliasili, Kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji ambayo itajadili maswala ya Urafiki wa Anga wa EAC. Aidha mbali na ripoti pia bunge litajadili miswada ya Mtangamano (Elimu) 2014,  Masuala ya Ushirika na Majadiliano ya Pamoja ya Biashara kwa Nchi wanachama.

Mbali na shughuli rasmi za bunge, Wabunge watatembelea taasisi mbalimbali ambapo tarehe 29 Agosti 2014 watatembelea  Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA), na Taasisi ya Sanaa  na Utamaduni (TASUBA) iliyopo Bagamoyo mnamo tarehe 30 Agosti 2014.

EALA imeazimia kufanya ziara hizi ili kuongeza ushirikiano baina ya EALA na washirika wake katika nyanja mbalimbali na kuboresha kazi za EALA katika utungaji wa sheria na mambo kadha wa kadha yanayoihusu jamii.

Wizara inawakaribisha wananchi kufuatilia kwa karibu vikao vya Bunge la Afrika Mashariki ili waweze kujua mambo mbalimbali yanayohusu mtangamano wa Afrika Mashariki.