Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LATEMBELEA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO. (TaSUBa).

 

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LATEMBELEA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa).

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki  (EALA) mwishoni mwa wiki walifanya ziara ya siku moja katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ili kujionea shughuli za Taasisi hiyo ambayo hivi karibuni ilipewa hadhi ya kuwa Taasisi Iliyobobea katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAM).

Ziara ya Wabunge hao iliongozwa na Spika wa EALA Mh. Dkt. Magreth Zziwa, ambapo walipokelewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Dkt. Fenella E. Mukangara pamoja na Uongozi wa TaSUBa.

TaSUBa ilipewa hadhi hiyo kwa lengo la  kupenyeza utamaduni miongoni mwa Nchi wanachama wa JAM. TaSUBa imepewa hadhi hiyo  ikiwa ni Taasisi pekee ya Sanaa na Utamaduni inayo ongoza kwa uwingi wa raslimali elimu, utamaduni na ubunifu katika JAM.

Wabunge wa EALA  walishiriki shughuli mbalimbali zilizoandaliwa na Taasisi hiyo ikiwa pamoja na upandaji miti, kukagua maeneo ya chuo, kushiriki michezo ya utamaduni na sanaa iliyo andaliwa na Taasisi hiyo.

Aidha Wabunge walipata fursa ya kutembelea jumba la kihistoria ambalo lilikua likitumiwa na watumwa kabla ya kusafirishwa kwenda kuuzwa Zanzibar.

Akitoa hotuba ya kuwakaribisha Wabunge Waziri Mukangara aliyeambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel, alisema shughuli za Sanaa na Utamaduni ni muhimu kwa nchi kwasababu zinatoa nafasi nyingi za ajira kwa Vijana.

Pia alitumia fursa hiyo kuwaomba Wabunge wa Bunge hilo kuelekeza nguvu nyingi kuwashawishi Wananchi wa Nchi wanachama kudumisha na kukuza Sanaa na Utamaduni.

Alisisitiza kuwa ni lazima utamaduni wetu uonekane katika nyanja mbalimbali za shughuli zetu za kila siku  katika jamii yetu pia aliwaomba wabunge wawashawishi vijana katika nchi zao wajiunge na TaSuBa.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mshariki Mh. Abdulla Juma Abdulla  Saadalla aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Joyce Mapunjo, aliwapongeza viongozi wa TaSUBa kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kukuza na kuendeleza sanaa na utamaduni.

Pia aliwataka viongozi wa Taasisi hiyo kubuni aina ya Lugha ya Kiswahili itakayo tumiwa na Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwakuwa kila nchi mwanachama haizungumzi Kiswahili kinachofanana.

“Kiswahili cha Zanzibar ni tofauti na cha Tanzania Bara, vilevile si sawa na cha Kenya na cha Uganda,” alisema Waziri.

Akizungumza kwa upande wake Spika wa Bunge la Afrika Mashariki  alitoa pongezi kwa uongozi wa TaSUBa kwa  kupewa hadhi ya kuwa Taasisi iliyo bobea pia kwa jitihada zao za kukuza Sanaa na Utamaduni katika Afrika Mashariki.

Zziwa aliongezea kusema kuwa anatambua kazi na mchango mkubwa wa hiyo katika kututambulisha watu Afrika Mashariki , kutuunganisha, na kukuza uchumi Afrika Mashariki.

 Aidha, aliahidi kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki itaendelea kuiunga mkono Taasisi hiyo katika kuitangaza Sanaa na Utamaduni Wetu.

EALA limejiwekea utaratibu wa kutembela Taasisi mbalimbali za nchi Wanachama watakazo tembelea, Taasisi zingine walizo tembela ni IPP Media na Bandari ya Dra-es-salaam.

EALA linaendelea na vikao vyake jijini Dar-es-salaam ambavyo  vitafikia tamati  August 2, 2014.