Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

JWTZ YAZOA VIKOMBE SITA MICHEZO YA MAJESHI YA EAC.

Mashindano ya nane (8) ya michezo ya majeshi ya Afrika Mashariki yaliyoaanza Agosti 18, 2014 katika viwanja vya Abeid Aman Karume Zanzibar yamalizika kwa mafanikio makubwa ambapo Tanzania imejizolea jumla ya vikombe sita. Mashindano haya yamefungwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda Agosti 29, 2014.

Mashindano ya nane (8) ya michezo ya majeshi ya Afrika Mashariki yanahusisha jumla ya Nchi tano za Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, mashindano haya yalianza kufanyika tangu mwaka 2006 na yamekuwa yakifanyika kila mwaka kwa mzunguko kwa kila Nchi ya Afrika Mashariki, kwa upande wa Tanzania hii ni mara ya pili mashindano haya yanafanyika Zanzibar, kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2007. Kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka huu ni ‘Jamii moja, Hatima moja kupitia michezo ya majeshi na utamaduni 2014’ na lengo kuu la michezo hii ni kuleta umoja kwa kuwakutanisha majeshi ya Afrika Mashariki kwa njia ya michezo ili kueendeleza amani na umoja kwa Nchi hizi. Jumla ya michezo minne ilishindindaniwa, michezo hiyo ni mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa mikono na mbio za nyika.

Tanzania imejinyakulia nafasi ya kwanza kwa mpira wa netiboli hii ikiwa ni mara ya nane wanakuwa vinara wa mchezo huo tangu kuanza kwa mashindano haya, vilevile Tanzania imeweza kupata nafasi ya kwanza mbio za nyika kwa wanaume, nafasi ya pili mpira wa miguu ambapo nafasi ya kwanza imechukuliwa na Kenya, nafasi ya nne mpira wa basketi, nafasi ya tatu mpira wa mikono na mlinda mlango wa timu ya mpira wa miguu Bw. Mwalimu kijogoo kujinyakulia kikombe cha mlinda mlango bora.

Akifunga michezo hii Mheshimiwa Pinda aliwapongeza sana kwa kuweza kudumisha ummoja huu kwa njia ya michezo na kusema michezo hii si kwa lengo la kushindana tu bali inajenga umoja na amani kati ya watu wa Nchi hizi tano, alisema “Iwapo majeshi yetu yataeendeleza utamaduni huu wa  kushirikiana, vita haitakuwa na nafasi kati yetu na tutaeendelea kudumisha amani katika nchi zetu” Mh. Pinda alisema ni jambo la kipekee kuwakutanisha majeshi matano ya Nchi tofauti na kukaa kwa pamoja kwa furaha na upendo kwa wiki mbili kwa kila mwaka kwa muda wa miaka minane sasa.

Jeshi la Tanzania limekabidhi bendera ya Afrika Mashariki kwa Uganda ikiwa ni ishara ya kukabidhi michezo kwa Jeshi la Uganda ambao wanatarajiwa kuandaa michezo hii mwakani, mkuu wa majeshi wa Tanzania Bw. Davis Mwamunyange alikabidhi bendera hiyo kwa Naibu Mkuu wa Majeshi wa Uganda Lt General Charles Angina na kuwatakia maandalizi mema ya michezo hii kwa mwaka 2015.

Na Robi Bwiru