Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

Karibu Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Mnazi Mmoja

                                                                                                              

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

 
   

TAARIFA KWA UMMA

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwataarifu wananchi wote kuwa inashiriki katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kuanzia tarehe 16 Juni, 2014 hadi 23 Juni, 2014 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.

Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda letu ili muweze kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara na kujifunza masuala muhimu yanayohusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Karibuni muweze kuongeza uelewa wenu kuhusu fursa mbalimbali zipatikanazo katika  mtangamano wa Afrika Mashariki, utaratibu wa kuuza na kununua bidhaa nchi za Jumuiya, miradi mbali mbali inayotekelezwa na Jumuiya, hatua za mtangamano na pia tutajibu maswali yenu.

 

Karibuni sana.

KATIBU MKUU

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI,

NSSF WATERFRONT GHOROFA YA 5,

35 BARABARA YA EDWARD SOKOINE

11467 DAR ES SALAAM

16-Juni-2014