Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

Miradi ya nishati inavyosaidia kutunza mazingira

Naibu Waziri  Wizara  ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt . Abdulla Juma Abdulla Saadala amesema Mradi wa kutengeneza  Majiko Banifu na Sanifu unaondelea katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka kilichopo Wilayani Maswa utachangia kwa kiasi kikubwa kunusuru uharibifu wa Mazingira katika vyanzo vya uhifadhi ya Maji ya Ziwa Victoria.

Alisema hayo wakati wa ziara yake  inayoendelea kukagua  miradi ya  maendeleo kwa Wananchi waishio kando ya mto Simiyu  inayofadhiliwa na LVEMP II ili kunusuru  chanzo hicho cha maji kinachopeleka maji yake katika Ziwa Victoria.

Aidha  ameridhishwa kwa kiasi kikubwa na faida na maendeleo ya mradi huu kwa Wananchi wa Malampaka kinyume na awali ambapo alikataa kuzindua mashine ya kuchakata alizeti ya Kijiji cha Kalulu nje kidogo ya Mji wa Bariadi.

Mradi huu unaofadhiliwa na Mradi wa kuifadhi Mazingira ya Ziwa Victoria awamu ya pili LVEMPII unaosimamiwa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania umekuja kama jibu la tatizo la utakataji miti kando kando ya mto Simiyu.

Majiko Banifu yanatumia rasilimali chache ya nishati ya kuni ambapo mtumiaji anatumia vipande vitatu vya kuni kwa matumizi ya nishati ya kupikia kwa siku moja na kiasi hicho hicho kikitumika hata kwa Taasisi zenye kuitaji matumizi ya kuni au mkaa mwingi  kama vile vyuo na Shule za bweni.

Dkt. Saadala pia alitembelea miradi ambayo ni mfano wa kinu cha  kutengeneza nishati ya gesi itokanayo na Samadi ya ng’ombe (biogas plant) uliopo Wilaya ya Itilima katika kijiji cha Ng’esha na mradi wa ufugaji nyuki uliopo katika Kijiji cha Madilana Wilayani hapo.

Miradi hii ya  LVEMPII chini ya Ufadhili wa Benki ya Dunia itachangia kwa kiasi kikubwa kunusuru mto Simiyu ambao ni Chanzo cha Maji ya Ziwa Victoria na kwa maeneo mengine yaliyo chini ya mradi huu uoto wa asili kando ya mto huu umeanza kurejea.