Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

MKUTANO WA 16 WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NAIROBI, KENYA.

Mkutano wa 16 wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa Kufanyika 20 Februari, 2015 Nairobi, Kenya katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa dharura wa  Baraza la Mawaziri la Jumuiya Jumuiya Afrika Mashariki. Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya  Afrika Mashariki unatarajia kufanya yafuatayo;

  • Kupitia taarifa ya Mwaka ya Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha Disemba 2013 hadi Novemba 2014,
  • Kupitia taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya Vikao vya Jumuiya ya Afrika     Mashariki
  • Kupitia taarifa ya Masuala ya kiutumishi yakiwemo; uteuzi wa Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Jumuiya Afrika Mashariki, Jaji wa Mahakama ya kwanza ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, uteuzi wa Naibu katibu Mkuu wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Burundi na kuongeza Muda wa Mkataba wa Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya kutoka Jamhuri ya Uganda.

Aidha katika Mkutano huu wa Wakuu wa Nchi wanatarajia kuzindua mpango wa kisasa wa kufanya Mikutano kwa Njia ya Video. (Video Confrence)

 

Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaotararijiwa kuhudhuria katika Mkutano huu ni Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Mhe. Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, Mhe. Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Mhe. Rais Paul Kagame wa Rwanda, na  Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye ni mwenyeji wa Mkutano.