Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

Mradi wa Mazingira wa Ziwa Victoria Mkombozi wa wananchi

Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira wa Bonde la Ziwa Victoria (LVEMP II) umekua mkombozi mkubwa wa mazingira kwa wananchi wa ukanda wa Ziwa, ikiwa pamoja na kudhibiti tatizo la magugu maji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mhe. Binilith Mahenge alisema mradi huo umeweza udhibiti magugu maji na uharibifu mwingine katika Ziwa Victoria, tatizo ambalo limekua sugu kwa muda mrefu.  

Aidha, Waziri Mahenge alisema LVEMP II imesaidia pia kudhibiti uharibifu wa viumbe viishivyo katika Ziwa hilo ambalo ni tegemeo la wananchi waishio karibu na ziwa.

Waziri Mahenge alikua akizungumza hivi karibuni katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza akiwa mgeni rasmi wa maonesho ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa inafanyika Jijini Mwanza.

Mradi huo ambao unasimamiwa na kuratibiwa na Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) mpaka sasa kwa upande wa Tanzania miradi midogo iloyochini ya mradi wa LVEMP II ipatayo 19 imekamilika na 197 iko katika hatua za utekelezaji.

Mradi wa LVEMP II ni mradi wa Jumuiya Afrika Mashariki ambao unatekelezwa katika Nchi tano(5) zinazogawana bonde la Ziwa Victoria ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

Akizungumzia miradi mbalimbali iliyo chini ya LVEMP II na mafanikio ya miradi hii kwa wananchi wanaolizunguka Ziwa hili na utunzaji wa mazingira

Bw.Msafiri Nashoni ambaye ni Ofisa mradi wa’Enviroment Management and Economic Development Organization’(EMEDOS) II ambao ni mradi  ulio chini ya LVEMP II, alitoa mfano wa mradi wa ‘Sustainable Energy and Economic Development’ (SEED) ambao ni mradi uliowezesha wananchi kutunza mazingira kwa kutumia gesi ya bioanuai.

Nashoni alisema gesi hiyo inayotengenezwa kwa mabaki ya maganda ya vyakula na mabaki yake na  baada ya kutengeneza gesi yanatumiwa kama mbolea.

Alisema lengo kuu la mradi huu ni kuendeleza shughuli mbalimbali zinazoweza kuinua kipato cha wananchi kwa kutumia njia ambazo ni rafiki wa mazingira.

LVEMP II ina miradi midogo inayoendeshwa na kusimamiwa na wananchi ipatayo 176 ambayo iko katika sehemu mbalimbali Tanzania mfano ni mradi wa ukarabati wa lambo katika kijiji cha Sayusayu mradi huu umenufaisha takribani wanakijiji 3, 628, tanki la uvunaji wa maji ya mvua katika kijiji cha Ipililo umenufaisha wanakijiji 890, upandaji wa miti katika kijiji cha Malita takribani miti 10, 000 imepandwa ndani ya mita 60 za mto Simiyu.

“Miradi hii pamoja na kuwa na lengo la kutunza mazingira lakini pia kwa kiasi kikubwa imesaidia kuleta maeendeleo katika vijiji vinavyojihusisha na miradi hii,” alisema Nashon

Kwa mujibu wa LVBC, katika kutekeleza mradi wa LVEMP II, matokeo 20 ya kikanda yaliyokubaliwa na nchi wanachama na mpaka sasa matokeo manne(4) yamekamilika, kumi na mbili (12) yanaeendelea kutekelezwa na manne(4) bado hayajaanza.

Mojawapo ya matokeo ya kikanda ni maandalizi ya miundo mbalimbali kwa ajili ya uanzishwaji wa mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira ya Ziwa Victoria (LVEF) na utambuzi wa vyanzo vya fedha.

Vilevile kuna mkakati wa udhibiti na usimamizi wa magugu maji uliopitishwa na  kamati ya kanda ya utekelezaji na kukubaliwa na baraza la kisekta la mawaziri wa LVB.

LVEMP II ina changamoto zake katika utekelezaji wa shughuli zake ambazo ni kama vile kwa mujibu wa LVBC, vikwazo dhidi ya utendaji bora, mzunguko mrefu wa miradi midogo inayoendeshwa na jamii, mchakato mrefu wa upitishaji wa miradi ya EAC, uwezo mdogo wa Wilaya katika kuratibu na kutekeleza miradi midogo katika sehemu zao.

Ili kutatua changamoto hii imeshauriwa kuwa kuna haja ya kukuza wigo wa mawasiliano na kujifunza ili kuziwezesha jamii kutoa mrejesho wa miradi mbalimbali, faida zake na ni jinsi gani wanatekeleza miradi hiyo.

Miradi hii imewanufaisha wanavijiji kwa kuwaongezea kipato kwa njia ambazo ni rafiki wa mazingira na kuwasaidia kuacha njia mbalimbali walizokuwa wanatumia hapo awali kujipatia kipato ambazo zinachafua mazingira hususani mazingira ya bonde la mto Simiyu ambao ni chazo kikubwa cha Ziwa Victoria.