Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

NAIBU WAZIRI AJIBU SWALI BUNGENI KUHUSU WABUNGE WA EALA

SWALI NA. 15

 

WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUTOA TAARIFA YA KAZI ZA BUNGE HILO BUNGENI

 

MHE. HERBRT JAMES MNTANGI (MUHEZA) Aliuliza:-

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio lenye jukumu la kutunga Sheria za Nchi, lakini hata hivyo Bunge la Afrika  Mashariki nalo linatunga Sheria zinazotumika katika nchi zote wanachama:-

 

a)      Je, kwanini Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki toka Tanzania wasipewe nafasi maalum ya kutoa taarifa ya kazi pamoja na sheria mpya ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

b)      Je, Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wanafanya vikao gani nchini ili kutoa elimu na maendeleo ya kazi na mwelekeo wa Jumuiya hiyo kwa ujumla.

 

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI Alijibu:-

 

Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki naomba kujibu swali la Mhe. Herbert James Mntangi, Mbunge wa Muheza, kama ifuatavyo:-

 

a)      Mheshimiwa Spika, Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulisainiwa na Nchi Wanachama tarehe 30 Novemba, 1999 na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria Na. 4 ya mwaka 2001 kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa Mkataba huo (Treaty for the Establishment of the East African Community Act No.4 0f 2001). Mkataba huo pamoja na mambo mengine umeainisha mfumo wa utendaji wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, na mahusiano kati ya Bunge la Afrika Mashariki na Mabunge ya Nchi Wanachama. Aidha, Bunge la Afrika Mashariki limetunga Kanuni ambazo zinaongoza utendaji kazi wa kila siku wa Bunge hilo na Wabunge wake

 

Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Tanzania Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nyongeza ya 4 ya kanuni, limeweka utaratibu wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania kuwasilisha taarifa za mara kwa mara kwenye Bunge la Tanzania. Kwa mujibu wa nyongeza hiyo, Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wanatakiwa kuwasilisha Taarifa ya Mwaka kuhusu shughuli zilizofanywa na Bunge la Afrika Mashariki kwa mwaka huo. Pamoja na Taarifa ya Mwaka, Wabunge hao wanaweza kuwasilisha Taarifa Maalum kila wanapoona kuwa ipo haja ya kufanya hivyo.

 

Mheshimiwa Spika, Aidha,Ibara ya 65 kifungu (a) – (d)  ya Mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inamtaka Katibu wa Bunge la Afrika Mashariki kuwasilisha nyaraka za majadiliano yote yaliyofanyika katika Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya Bunge hilo kumaliza mkutano wake katika Mabunge ya Nchi Wanachama zikiwemo sheria mpya zilizotungwa na nyaraka hizo zitawekwa mezani na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 

b)      Mheshimiwa Spika, Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wana wajibu wa kuhakikisha kuwa elimu juu ya Mtangamano wa Afrika Mashariki inafika kwa jamii nzima. Katika kuteleza azma hii Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wamekuwa wakifanya ziara mbalimbali (Outreach Programs) katika maeneo kama Mipakani, Bandarini nk zenye lengo la kuelimisha wananchi kuhusu Jumuiya ya Afrika Mshariki.

 

Aidha, utaratibu umewekwa wa kuendesha Bunge la Afrika Mashariki kwa mzunguko miongoni mwa nchi wanachama ili kutoa fursa kwa Wabunge na Wananchi kwa jumla kupata nafasi ya kujua maendeleo katika Jumuiya. Vilevile Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wamekuwa wakifanya vikao na mikutano na taasissi mbalimbali kwa lengo la kuelezea maendeleo na mwelekeo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.