Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

SALAMU ZA POLE KWA MSIBA

Uongozi na Wafanyakazi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki unatoa pole kwa Katibu Mkuu wake Bi. Joyce K.G. Mapunjo kufuatia kifo cha Mume wake Profesa Zakaria Mmbwambo (58) kilichotokea Jumamosi tarehe 19 Julai 2014, Dar es Salaam.

Wizara inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kuipa mkono wa pole familia ya Profesa Mmbwambo katika kipindi hiki kigumu.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Ratiba ya Maombolezo na Mazishi ni kama ifuatavyo:

1: LEO JUMATATU JULAI 21, MWILI WA MAREHEMU UTAAGWA MUHIMBILI NA WAFANYAKAZI WENZAKE SAA 6 MCHANA KWA MAANDAMANO YA WANATAALUMA NA HESHIMA ZA MWISHO ZITATOLEWA SAA 7 MCHANA MUHAS. BAADA YA HAPO MWILI UTAPELEKWA NYUMBANI KWAKE OYSTERBAY NA KUTOLEWA RAMBIRAMBI SAA 8 MCHANA. SAA 11 JIONI  MWILI UTAPELEKWA KIMARA STOP-OVER NYUMBANI KWAKE PIA.

2: KESHO JUMANNE JULAI 22, MWILI UTAKUWEPO NYUMBANI KWAKE KIMARA NA MAOMBOLEZO NA RAMBIRAMBI ZITAANZA SAA 4 ASUBUHI NYUMBANI KWA MAREHEMU, SAA 7 MCHANA MWILI UTAPELEKWA KANISANI KIMARA LUTHERAN CHURCH KWA AJILI YA SALA SALAMU ZA MWISHO. SAA 10 JIONI MWILI UTAPELEKWA NYUMBANI KWA MAZISHI.