Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

Serikali kujenga jengo la muda Tunduma kurahisisha biashara

Serikali imesema itajenga jengo la muda kwa ajili ya abiria na mizigo katika Mpaka wa Tunduma wakati ikisubiri kukamilika kwa jengo la Utoaji wa Huduma za Pamoja Mipakani (One Stop Boarder Post).

Mpaka wa Tunduma, ambao upo kati ya Tanzania na Zambia, ni mkubwa kibiashara kuliko mipaka yoye Nchini ikipitisha zaidi ya asilimia 30 za mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza katika hotuba yake ya mwisho mwa Februari 2015, Rais Dkt. Jakaya Kikwete alisema Tanzania imekubaliana na Zambia kujenga jengo hilo ili kurahisisha upitishaji wa mizigo.

“Kuhusu kuboresha huduma kwa abiria na mizigo katika mpaka wa Tanzania na Zambia pale Tunduma, tumekubaliana kuwa, Serikali ya Tanzania ikamilishe ujenzi wa jengo  litakalowezesha huduma zote muhimu za mpakani kutolewa katika jengo hilo (One Stop Border Post).

 Wakati tunasubiri kukamilisha ujenzi huo, tumekubaliana tuwe na jengo la muda la kurahisisha taratibu za usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo katika mpaka wetu na Zambia, alisema Rais akizungumzia Ziara yake ya Zambia hivi karibuni.

Rais Kikwete alisema vilevile, katika ziara hiyo walizungumzia njia za kuimarisha na kuboresha taratibu za forodha kwa mizigo itokayo bandari ya Dar es Salaam kwenda Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Zambia. 

“Tumekubaliana kuwa, Mamlaka ya Kodi ya Mapato ya Zambia iangalie uwezekano wa kuwaweka maafisa wake katika Bandari ya Dar es Salaam kama inavyofanyika kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema Rais

Alisema hatua hiyo itarahisisha taratibu za forodha kwa bidhaa za Zambia katika bandari ya Dar es Salaam.

Alidokeza kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeshaanza mchakato wa kupata fursa ya kuwa na maofisa wake Bandari ya Dar es Salaam.

Mwisho.