Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

TANZANIA KINARA AMANI, UTULIVU NA UTAWALA BORA - AFRIKA.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara nyingine tena ameudhihirishia ulimwengu hasa ukanda wa Afrika Mashariki kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani kwa kutunikiwa nishani ya Amani na Utulivu kutoka Kampuni ya East Africa Book of Records yenye makao makuu yake nchini Uganda.

Akimkabidhi tuzo hiyo Mtendaji mkuu wa Kampuni hiyo Dkt.  Paul Bamutize alisema ‘Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa hasa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, vilevile alikipongeza chama cha mapinduzi kwa kusimamia vyema Amani hiyo hapa Nchini”. Dkt. Bamutize alimpongeza sana Mhe. Rais Kikwete na kuelezea kuwa amani ya Tanzania imechangia sana kuvutia  wawekezaji kutoka nje na hata kwa majirani wanaoizunguka na hivyo kufanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa na majirani zake kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Mhe.Rais alisema “Amani hii tuliyonayo hapa nchini imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania ambao napenda kupokea nishani hii kwa niaba yao kwa sababu wao ndio watunzaji na walinzi wa Amani hii”

Sambamba na hilo Mhe. Rais Kikwete  Julai 25,2015 alitunikiwa tuzo kubwa Afrika ya Uongozi na Utawala bora (Africa Archiever’s Award), tuzo hiyo ilitolewa Nchini Afrika Kusini na ilipokelewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. AshaRose Migiro kwa niaba ya Rais.

Mhe. Rais anakuwa Mwafrika wa Nne(4) kupata tuzo hiyo, tuzo hiyo imewahi kutolewa kwa Rais wa zamani wa Ghana, Hayati John Atta Mills, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mama Nkozana Dlamini Zuma na aliyekuwa kiongozi wa Kanisa la Anglikana na mwanaharakati Mashuhuri wa Afrika Askofu Mkuu Desmond Tutu. Mhe. Rais aliibuka kidedea baada ya kuwashinda jumla ya Waafrika Mashuhuri 1,201 ambao majina yao yalipendekezwa kwa ajili ya kutunikiwa tuzo hiyo.

Miongoni mwa vigezo vilivyopelekea Mhe. Rais kushinda tuzo hiyo ni jinsi alivyosimamia utawala wa Sheria, alivyoachangia kujenga demokrasia nchini, mapambano na rushwa na kuheshimu haki za bianadamu. Aidha, akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Mhe. Migiro, Ikulu, Mhe. Rais alisema ““Mimi naipokea tuzo hii kwa niaba ya Watanzania. Wao ndio washindi wa kwelikweli wakiongozwa na Serikali yao ambayo imefanikisha kudumisha utawala bora katika miaka 10 iliyopita.Wenzetu wametupima kwa kutulinganisha na wengine na tukaonekana bora. Nawashukuru sana kwa imani yao kwetu.”

Mhe. Rais alisema hakuweza kwenda kupokea tuzo hii muhimu kwa sababu alikuwa kwenye ziara ya Kiserikali nchini Australia, Mhe. Rais alieleza ni jinsi gani amefurahi kupokea tuzo hiyo.

 

---------------------- Mwisho-----------------------------