Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

Wafanyabiashara Namanga waomba kujengewa soko

Wafanyabiashara wa Namanga na maeneo mengine ya Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha wameiomba Serikali iwajengee Soko kubwa eneo la Namanga ili waepukane na usumbufu wanaoupata wanapokwenda Kenya kuuza mifugo, mazao na bidhaa nyingine.

Wafanyabiashara hao walitoa ombi lao jana Septemba 19 wakati wa mkutano na Maofisa wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wanaotembelea mipaka mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya Mtangamano wa Afrika Mashariki.

Baadhi ya manyanyaso wanayopata wanadai ni kuombwa kitu kidogo, kupewa malipo kidogo ya bidhaa zao kuliko bei ya soko na kusumbuliwa kuhusu ubora wa bidhaa wakati bidhaa zao zimetimiza viwango vyote.

Uongozi wa Wilaya ya Longido umetenga eneo la heka 120 kwa ajili ya soko ili wafugaji na wakulimna wauzie bidhaa zao hapo.

Uwepo wa soko pia utasaidia Wanunuzi kutoka Kenya waje kununua sokoni hapo na hivyo wakulima na wafanyabishara wa Tanzania kupata bei nzuri na kuepuka usumbufu wanaoupata sasa.

Wafanyabishara hao pia wamesema ujenzi wa soko utasaidia kuzuia Wakenya kwenda mashambani na kununua mazao moja kwa moja kwa wakulima.

Akizungumza na wafanyabiashara hao Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Graceana Shirima alisema Serikali itashugulikia haraka malalamiko yao ikiwa pamoja kuharakisha ujenzi wa masoko mipakani.

Shirima, ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Joyce Mapunjo, alishauri uongozi wa Wilaya ya Longido kuanza na utaratibu wa gulio wakati wakiendelea na mikakati ya ujenzi wa soko.

Mweka Hazina wa Wilaya Issai Mbiru alisema tayari Wilaya imepata fedha Shilingi bilioni 2.3 kutoka kwa wafandhili na ujenzi wa soko hilo utaanza muda si mrefu.