Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

WAJUMBE WAPYA WAWILI WAAPISHWA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

WAJUMBE WAPYA WAWILI WAAPISHWA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (BJAM) katika Mkutano wake wa pili (2), kipindi cha Nne (4) cha Bunge la tatu linaloendelea Jijini Nairobi; tarehe 7 Oktoba , 2015 lilisimamia kiapo cha utii wa Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wajumbe wapya wawili (2) waliojiunga na Bunge hilo.

Bunge lilimwapisha Waziri  wa Wizara ya Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Burundi Mhe. Leontine Nzeyimana ambaye ameteuliwa tena kuiongoza Wizara hiyo.

Mhe. Dkt. Francois Xavier Kalinda, ambaye ni Mbunge mpya toka Nchini Rwanda pia aliapishwa katika Mkutano huo, kiapo kiliongozwa na Katibu wa BJAM Bw. Kenneth Madete mbele ya Spika wa Bunge hilo Mhe. Daniel F. Kidega.

Wote wawili waliapa kwa mujibu wa kanuni ya 5 (4) ya Kanuni za Bunge la BJAM inayosema; “Hakuna Mbunge anaweza kukaa au kushiriki katika vikao vya Bunge mpaka hapo kiapo cha kudhihirisha utii kwa Mkataba kitakapo chukuliwa" (No Member can sit or participate in the proceedings of the House until the Oath or Affirmation of Allegiance to the Treaty is taken”)

Kabla ya kuchaguliwa na Bunge la Rwanda na kuapishwa kuwa Mbunge wa BJAM Mhe. Dkt. Kalinda, alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Rwanda. Mhe. Dkt Kalinda ameapishwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Celestine Kabahizi ambaye alijiuzulu Juni, 2015.

Aidha, Mhe. Leontine Nzeyimana, ameteuliwa kwa mara nyingine kuwa Waziri wa Wizara ya Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufuatia uchaguzi  uliofanyika Mwezi Julai Nchini Burundi. Mhe. Nzeyimana ameiongoza Wizara katika nafasi hiyo tangu mwaka 2012. Mhe. Nzeyimana ana Shahada ya Uzamili katika Mahusiano ya Kimataifa, ambapo kabla alisoma Shahada ya Usimamizi wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, Tanzania aliyohitimu mwaka 2002.