Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

WAZIRI AFUNGUA MILANGO KWA MAWAKALA WA UTOAJI NA USAFIRISHAJI MIZIGO.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe amefungua milango kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Tanzania kushirikiana na Wizara katika kuhakikisha nchi inafaidika na fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akizungumza na baadhi ya Wanachama Chama cha Mawakala wa Utoaji na Usafirishaji Mizigo Tanzania (TAFFA) jana Waziri Mwakyembe alisema Serikali inatambua mchango wa Mawakala hao katika kuchangia ukuaji wa uchumi wan chi.

“Kwa kutambua umuhimu wenu napenda kuwakaribisha Wizarani wakati wowote mtakapohitaji msaada kutoka kwetu pia napenda kutoa wito kwenu msisite kushirikiana nasi wakati wowote tunapohitaji ushauri kutoka kwenu kwa lengo  la kuimarisha utendaji” Waziri Mwakyembe alisema

Kauli hii imetolewa jana na Mhe.  Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe alipokutana na Wanachama wa Chama cha Utoaji na Usafirishaji Mizigo (Tanzania Freight Forwarders Association. TAFFA) katika Kikao kifupi kilichofanyika Wizarani.

Katika kikao hicho Kifupi Mhe. Waziri aliwataka Wanachama wa TAFFA wakiongozwa na Rais wao Bw. Stephen Ngatunga, kueleza vikwazo vinavyo wakumba katika kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Waziri alisema inaonekana Mawakala Wautoaji na Ushafirishaji Mizigo wa Tanzania wanashindwa kukabiliana na kasi ya Ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania zinasema Nchini kuna idadi ya Kampuni 524 zilizosajiliwa kisheria na kupewa leseni ya kuendesha Biashara ya kutoa na kusafirisha mizigo.

Katika kikao hicho wanachama wa TAFFA walieleza matatizo na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kukabiliana na ushindani wa kibiashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Moja ya changamoto kubwa waliyoitaja ni uwepo wa Sheria inayowataka kuhuisha leseni zao za biashara kila baada ya mwaka mmoja.

“Sheria hii imekuwa ni kikwazo kikubwa kwetu inatunyima fursa ya kukopa ili kukuza mitaji yetu itakayo tuwezesha kukabiliana na kasi ya ushindani wa kibiashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki” alisema Rais wa chama hicho na kupendekeza kuwa Sheria hiyo ifanyiwe marekebisho ili iwaruhusu kuhuisha leseni zao za biashara kila baada ya miaka mitano.

Wanachama wa TAFFA walitumia fursa hiyo kumuomba Mhe. Waziri awasadie kutatua kero zao na kuzifikisha kwa Taasisi husika ikiwa ni pamoja na kufanya Mkutano wa pamoja na Taasisi hizo utakao wakutanisha Mhe. Waziri TAFFA na Taasisi husika zikewemo TRA na Wizara ya Fedha.

Mhe. Waziri aliahidi kuyafanyia kazi masuala yote yaliyojadiliwa na kuafikiwa katika kikao hicho.