Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

Hongera Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kumpongeza Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, kwa kuteuliwa na Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo katika Mkutano wa Viongozi Wakuu hao tarehe 18 Agosti, 2013, Jijini Lilongwe, Malawi.

Uteuzi wa Mhe. Dkt. Tax katika wadhifa huo mkubwa na nyeti sio tu ni fahari kwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambako amekuwa Katibu Mkuu, bali pia kwa atanzania wote. Tanzania kama mmoja wa nchi waanzilishi wa SADC na mshirika muhimu, inajisikia fahari kwa kushika nafasi hii ya Katibu Mtendaji. Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax anaondoka akiwa na mafanikio makubwa katika Uendelezaji wa Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inamtakia, Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax, kila la kheri katika majukumu yake mapya na inajivuna kwamba SADC imepata Kiongozi shupavu, mahiri na mchapa kazi.

File Attachment: