Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI

Mkutano wa 32 wa Baraza la Mawaziri unatarajiwa kufanyika kesho tarehe 14 Agosti,2015 Jijini Arusha Tanzania. Mkutano huu wa Baraza la Mawaziri unafanyika kesho ukiwa umetanguliwa na Vikao vya Maafisa Wandamizi wa Serikali na Kamati ya Uratibu (Makatibu Wakuu) ambavyo vilifanyika kuanzia tarehe10 hadi 13 Agosti, 2015.

Pamoja na mambo mengine Baraza la Mawaziri litajadili na kuzingatia mambo yafuayo;

  • Taarifa ya Tume ya Ukaguzi
  • Taarifa ya utekelezajia wa mazimio yalifanywa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliopita
  • Taarifa ya Mkutano wa 22 wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wanaosimamia masuala na mipango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
  • Taarifa ya Kikosi kazi cha ngazi ya juu kinacho shughulikia masuala ya marekebisho ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Vilevile moja ya ajenda itakayo jadiliwa katika Mkutano huu wa 32 wa Baraza la Mawaziri itahusu Mkutano wa kwanza wa Kilele wa Wafanyabiashara wanaomiliki Viwanda vya Uzalishaji uanaotarajiwa  kufanyika Jijini Kampala, Uganda tarehe 1 hadi 2, Septemba 2015.

Aidha, Baraza litajadili na kuzingatia ripoti kutoka taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo ripoti ya Taasisi ya Shirikisho la Vyuo Vikuu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki

Imetolewa na;

Katibu Mkuu

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI