Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

Pongezi kwa Vyeo

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwapongeza afanyakazi wake wanne kwa kupandishwa vyeo na kushika nyadhifa za Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu katika Wizara mbalimbali.

Waliopandishwa vyeo ni pamoja na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bw. Uledi A. Mussa, Bw. Armantius C. Msole (Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji), Bibi Rose Shelukindo (Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu) na Bw. Edwin K. Kiliba (Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama).

Bw. Uledi A. Mussa anakua Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Armantius C. Msole anakua Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Rose Shelukindo anakua Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Bw. Edwin K. Kiliba anakua Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Aidha, Wizara inampongeza na kumkaribisha Wizarani Bibi Joyce Mapunjo kwa kuteuliwa kwake kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wizara inawatakia wote kila la kheli katika nyadhifa zao mpya.

File Attachment: