Fri 30, Oct 2015 at 17:51:29   |  Rais akutana na waangalizi wa Uchaguzi kutoka EAC
Thu 13, Aug 2015 at 16:11:06   |  MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI
Fri 29, May 2015 at 13:15:10   |  HOTUBA YA BAJETI MEAC 2015/2016
Mon 23, Feb 2015 at 10:29:11   |  PRESIDENT SPEECH EAC SUMMIT FEB 20, 2015
Mon 17, Nov 2014 at 16:38:03   |  EALA to Hold Plenary in Nairobi Next Week
Mon 08, Sep 2014 at 11:36:07   |  House Passes Key Resolution on PWDs

WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA EAC WAHIMIZWA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU NCHINI

WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA EAC WAHIMIZWA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU NCHINI

Kuelekea uchaguzi Mkuu Nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 Jumuiya ya Afrika Mashariki imeleta timu ya waangalizi yenye jumla ya watu 55 inayohusisha wataalamu na viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwemo wastaafu  na wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi wanachama. Timu hii iliwasili Jijini Dar es Salaam 18 Oktoba, 2015.

Katibu Mkuu  Bibi Joyce Mapunjo akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam ambao pia ulihudhuriwa na waangalizi kutoka EAC na SADC amewahimiza waangalizi wa uchaguzi kuzingatia sheria na taratibu za Nchi katika shughuli zao.

Akizungumza katika mkutano huo alisisitiza kuwa Tanzania ni Nchi ya Kidemokrasia na inautaratibu mzuri wa kuachiana madaraka ambapo uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka mitano na kubadilsha uongozi wa juu kila baada ya miaka kumi kwa mujibu wa katiba.

Kiongozi wa timu ya Uchunguzi kutoka EAC ambaye pia ni Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya Mhe. Dkt. A. A Mood Awori akizungumza katika Mkutano huo aliipongeza Tanzania kwa kudumisha Demokrasia na Utawala wa kisheria na kuongeza kuwa katika uchaguzi huu Tanzania iendeleze utamaduni wa kudumisha Demokrasia, Utawala Bora na uwajibikaji ili iendelee kuwa na amani na utulivu.

Timu ya waangalizi ya EAC ambayo itafanya kazi katika vipindi vitatu vinavyotajwa kuwa, Kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi itaangalia mambo yafuatayo;

  • Ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika kuripoti masuala mbalimbali ya uchaguzi
  • Muda wa kutosha wa  kampeni
  • Uhuru wa kuendesha shughuli za kisiasa pasipo fujo au vitisho
  • Utolewaji wa elimu ya uraia na upigaji kura
  • Upigaji kura kwa siri, na
  • Ubora wa vifaa vya uchaguzi

Aidha timu hiyo ya waangalizi itafanya kazi yake Tanzania bara na Visiwani wakati wote wa uwepo wake katika kipindi chote cha uchaguzi.